Herunterladen Inhalt Inhalt Diese Seite drucken

Briggs & Stratton 1150 Serie Original Bedienungsanleitung Seite 176

Inhaltsverzeichnis

Werbung

Verfügbare Sprachen
  • DE

Verfügbare Sprachen

  • DEUTSCH, seite 39
Ukarabati
Utaratibu wa Ukarabati
Fuata vipimo vya kila saa au kalenda, vyovyote vile vinavyokuja
mbele. Huduma ya mara kwa mara zaidi inahitajika wakati
unapoendesha kwenye hali mbaya zaidi.
Saa 5 za Kwanza
• Badilisha mafuta (oil) ya injini
Kila baada ya Saa 8 au Kila Siku
• Safisha chembechembe
• Kagua kiwango cha mafuta (oil) kwenye injini
Kila baada ya Saa 25 au Kila Mwaka
• Hudumia kisafishi cha hewa kwenye injini
Kila baada ya Saa 50 au Kila Mwaka
• Badilisha mafuta (oil) ya injini
• Kagua mafla
Kila baada ya Saa 100 au Kila Mwaka
• Plagi ya mwake ya kuhudumiwa
• Mfumo safi wa kupoza
1
Huduma hupatikana mara nyingi katika hali chafu au zenye vumbi.
Mapendekezo ya Jumla
Ukarabati wa mara kwa mara utaboresha utendakazi na
kurefusha maisha kwa kioshaji kwa presha. Tazama wauzaji
wengine wa Utoaji Huduma huu Walioidhinishwa wa Briggs &
Stratton kwa kupata huduma.
Udhamini wa kioshaji kwa presha haujumlishi vitu, ambavyo
vimetumiwa vibaya au kupuuzwa na anayevitumia. Ili kupokea
thamani kamilifu kutoka kwenye udhamini huu, mtumizi lazima
akihifadhi kioshaji kwa presha kama alivyoelekezwa katika
kabrasha ili ukiwemo uifadhi kamilifu kama ulivyoelezewa katika .
ONYO Ili kuhakikisha usalama wa mashine, tumia tu vipuri
(spare parts) asilia kutoka kwenye mtengenezaji au mtengenezaji
aliyeidhinishwa. Endapo utakuwa na maswali yoyote kuhusu
kusawazisha vipuri hivi kwenye kioshaji kwa presha chako,
tafadhali tembelea tovuti yetu katika BRIGGSandSTRATTON.COM.
Mpira wa Ukaguzi wa Ufyonzaji Sabuni
Mara kwa mara kagua mpira kwenye mfumo wa ufyonzaji sabuni
ambao unaweza kukwama kwenye uifadhi, sabuni iliyokauka au
madini yaliyomo ndani ya maji. Mpira huo wa ukaguzi unaweza
kukarabtiwa kwa kutekeleza yafuatayo:
1. Zima chanzo cha maji.
2. Ukiwa umezima injini na kuwachilia presha kutoka kwenye
mfumo, ondoa mpira wa maji unaofyonza sabuni kutoka
kwenye sehemu husika katika pumpu.
3. Kwa kutumia kifaa butu, kilichodhabiti chenye kipenyo
cha 2mm (7/64") au ndogo zaidi kwa angaa 25.4mm (1")
kwa urefu, kama vile Allen Wrench, chomeka kifaa hicho
polepole kwenye sehemu husika mpaka pale ambapo
utakapopata upinzani. Upinzani huo ndio mpira huu wa
ukaguzi.
4. Sukuma polepole mpaka pale ambapo utahisi mpira huo
ukisonga polepole,usisukume zaidi ya 3mm (1/8"). Presha
kidogo inaweza kuhitajika ili kuachilia mpira huo.
5. Rudia hatua za 4 na 5 kama itahitajika.
6. Weka upya mpira wa maji wa kufyonza sabuni kwenye
sehemu husika.
7. Tia dawa kwa kutumia PumpSaver kama ilivyofafanuliwa
katika Kuilinda Pampu wa uifadhi ili kuzuia kuepuka hali hiyo
kutokea tena.
8
8
1
1
1
Ukarabati wa Ncha ya Mnyunyizo Mchoro 5
Safisha nje ya mnyunyizo ili kusahihisha presha ya kupindukia ya
pampu iliyosababishwa na ncha ya mnyunyizo iliyo fungamana:
1. Zima chanzo cha maji.
2. Ondoa ncha ya mnyunyizo kutoka kwenye sehemu ya
mwisho ya kirefusho cha pua.
3. Tumia klipu ndogo ya karatasi ili kuondoa chembechembe
zozote za kigeni ambazo zimeziba au zinazuia njia hiyo ya
mnyunyizo (B).
4. Weka upya ncha hiyo ya mnyunyizo kwenye kirefusho
cha pua.
Ukarabati wa Pete-O Mchoro 12
Matumizi ya kilainisho (mafuta au grisi iliyotengenezwa)
husaidia kuweka pete-O hizo vyama na kuboresha namna
vinavyofunga sehemu hiyo. Paka kilainishi kwenye pete-O kabla
ya kuunganisha mpira wa maji bustanini kwenye pampu (A),
(B), mpira wa maji wa presha ya juu (C), sehemu ya mbele ya
mnyunyizo na kirefusho cha pua (D).
Nunua Mkoba wa Ukarabati wa Pete-O kwa Kuwasiliana na
Mwuzaji wa Aliyeidhinishwa kwa kutoa Huduma wa Briggs &
Stratton. Rejelea karatasi ya maelekezo iliyotolewa kwenye
mkoba huu ili kukarabati kitengo chako cha pete-o. USIWAHI
kukarabati miunganisho inayovuja kwa kinatishi cha aina yoyote.
Sawazisha pete-o au kinatishi.
Uhifadhi
Kama upangilii kutumia kioshaji kwa presha kwa zaidi ya siku 30,
lazima utayarishe injini na pampu kwa kuhifadhiwa.
Kuilinda Pampu
Ili kuilinda pampu dhidi ya uharibifu unaosababishwa na mabaki
ya madini au kuganda, tumia PumpSaver ili kuzuia uharibifu wa
kuganda na kulainisha pistoni na vinatishi.
ARIFA Kushindwa kulinda kitengo hiki dhidi ya halijoto ya
kuganda kutaweza kuharibu pampu na kufanya kitengo hiki
kutoweza kufanya kazi. Uharibifu wa kuganda haujajumulishwa
kwenye udhamini.
Kulinda Mfumo wa Mafuta
Mafuta yanaweza kuharibika endapo yatahifadhiwa zaidi ya siku
30. Mafuta yaliyoharibika yanaweza kusababisha mabaki ya asidi
na gamu na kufanya mabaki haya kubakia kwenye mfumo wa
mafuta au kwenye sehemu muhimu za kabyureta.
Hakuna haja ya kuondoa mafuta kutoka kwenye injini kama
kidhibiti cha mafuta kitaongezwa kulingana na maelekezo
yaliyotolewa. Endesha injini kwa dakika 2 ili kuzungusha kidhibiti
kwenye mfumo wote wa mafuta kabla ya uhifadhi.
Kama mafuta kwenye injini hayajatiwa dawa kwa kutumia kidhiti
cha mafuta, lazima yaondolewe na kuwekwa kwenye mkebe
ulioidhinishwa. Endesha injini mpaka pale itakaposita kutokana
na ukosefu wa mafuta. Matumizi ya kidhibiti cha mafuta kwenye
mkebe wa kuhifadhi yanapendekezwa ili kuhakikisha mafuta hayo
ni mazuri.
Vidokezo Vingine vya Uhifadhi
1. USIHIFADHI mafuta kutoka kwenye msimu mmoja hadi
mwingine isipokuwa tu kama yametiwa dawa kama
ilivyofafanuliwa katika Linda Mfumo wa Mafuta.
2. Funika kitengo hiki kwa kifuniko kinachofaa cha ulinzi
ambacho hakibakishi unyevunyevu.
ONYO! Fifuniko vya uhifadhi vinaweza kusababisha moto
na hatimaye kifo au majeraha mabaya. USIWEKE kifuniko
cha uhifadhi juu ya kioshaji kwa presha chenye joto.
Hakikisha kwamba mitambo hii imepoa kwa muda unaotosha
kabla ya kuweka kifuniko kwenye mitambo hii.
3. Hifadhi kitengo hicho katika eneo safi, kavu.
BRIGGSandSTRATTON.COM
BRIGGSandSTRATTON.COM

Quicklinks ausblenden:

Werbung

Inhaltsverzeichnis
loading

Diese Anleitung auch für:

Elite 3400Bpw3400020595-02

Inhaltsverzeichnis