Herunterladen Inhalt Inhalt Diese Seite drucken

Briggs & Stratton Q6500 Anleitung Seite 199

Inhaltsverzeichnis

Werbung

Verfügbare Sprachen
  • DE

Verfügbare Sprachen

  • DEUTSCH, seite 44
ILANI Injini ikikosa kuwasha, sukuma ndani kidhibiti cha choki
na urudie hatua ya 4. Injini ikiwasha lakini ikose kunguruma,
tazama Kiashiria Oili Chache.
QPT (QUIET POWER TECHNOLOGY) Kielelezo 1
Kipengele hiki inaimarisha utumizi wa mafuta. Wakati swichi ya
QPT (1, D) IMEWASHWA (ON), kasi ya injini itaongezeka kadri
vifaa vinavyotumia umeme vinapounganishwa, na kupunguka
kadri vifaa vinavyotumia umeme vinapoondolewa.
Swichi ikiwa imezimwa, injini itanguruma kwa kasi zaidi.
Hatua ya 4: Kuunganisha Vifaa
Vinavyotumia Umeme
Kurejesha Nishati Nyumbani kwa Kutumia
Swichi ya Ubadilishaji
Uunganishaji kwenye mfumo wa umeme wa nyumba yako ni
lazima utumie swichi ya ubadilisha isiyo otomatiki iliyowekwa
na fundi wa umeme aliyehitimu. Muunganisho huu ni lazima
utenganishe nishati ya jenereta na umeme wa kawaida na
uambatane na sheria na kanuni zote husika za umeme.
Kurejesha Nishati kwa Kutumia Kebo Ndefu
Matumizi ya umeme ya jenereta hii, hayafai kupita uwezo
wa nguvu za umeme zilizopendekezwa, katika hali
iliyopendekezwa, kama ilivyoonyeshwa kwenye lebo ya data ya
kifaa. Punguza matumizi ya umeme unapotumia jenereta katika
hali ambazo hazijapendekezwa.
Tumia nyaya-enezi za ubora wa juu kuambatana na IEC 60245-
4 na nyaya za kutoa umeme za kutoa umeme wa AC kwenye
jenereta za volti 230. Kagua nyaya-enezi kabla ya kila tumizi.
Hakikisha kwamba nyaya-enezi zote zina vipimo mwafaka na
hazijaharibika. Unapotumia nyaya-enezi chini ya 40° C, jumla
ya urefu wa nyaya kwa sehemu ya msalaba ya 1.5 mm² haifai
kuzidi mita 60 au kwa sehemu ya msalaba ya 2.5 mm² haifai
kuzidi mita 100.
ONYO! Nyaya-enezi zilizozidisha kiwango cha
vitumizi zinaweza kupata joto kubwa, kupinda, na
kuchomeka na kusababisha kifo au majeraha
mabaya.
• Vifaa vya elektroniki, pamoja na kebo na vizibo vya
kuunganisha, havifai kuwa na hitilafu.
1. Weka ving'ora vya kaboni monoksidi.
2. Unapoendesha jenereta ukitumia kebo ndefu, hakikisha
ipo mahali wazi, nje, angalau mita 6.1 mabla na mahali
kuna watu na ekzosi ikiwa umeelekezwa mbali.
3. Kebo ndefu zinazoelekea moja kwa moja hadi ndani
ya nyumba, na kuendesha vifaa vya ndani ya nyumba
HAIPENDEKEZWI.
ONYO! Eksozi ya injini ina kaboni monoksidi,
gesi ya sumu ambayo inaweza kukuua kwa dakika
chache. Hauwezi kuinusa, kuiona, wala kuionja. Hata
kama huwezi kunusa mafukizo yanayotolewa, bado
unaweza kupumua gesi ya monoksidi ya kaboni.
• Kebo ndefu zinazoelekea moja kwa moja hadi ndani ya
nyumba zinaongeza hatari kwako ya sumu ya kaboni
monoksidi kupitia mianya.
• Iwapo kebo ndefu inayoelekea moja kwa moja hadi ndani ya
nyumba inatumika kuendesha vifaa vya umeme vilivyo ndani
ya nyumba, mwendeshaji anatambua kwamba hili linaongeza
hatari ya sumu ya CO kwa watu walio ndani ya nyumba na
anawajibikia hatari hiyo.
4. Weka swichi ya ubadilishaji isiyo otomatiki punde
iwezekanavyo iwapo jenereta itatumiwa kurejesha nishati
nyumbani.
Plagi za Volti 230 za AC, Amp 16
Tumia plagi ili kuendesha vifaa vya umeme vya Volti 230 za
AC, msururu mmoja, 50 Hz vinavyohitaji hadi wati 3,680 (kW
3.68) katika umeme wa Amp 16.
ONYO! Volti za jenereta zinaweza kusababisha
mshtuko wa umeme au kuchomeka kunakoweza
kusababisha kifo au majeraha mbaya.
• Usiguze nyaya au plagi zilizo wazi.
• Usitumie jenereta yenye nyaya za umeme ambazo
zimechakaa, kuchubuka, wazi au vinginevyo zilizoharibika.
• Usitumie jenereta kwenye mvua au wakati kuna
unyevunyevu.
• Usishike jenereta au nyaya za umeme ukiwa umesimama
ndani ya maji, ukiwa miguu mitupu ama mikono na miguu
ikiwa na maji.
• Usiruhusu watu ambao hawajahitimu au watoto kuendesha
au kuhudumia jenereta.
• Weka watoto mahali salama mbali na jenereta.
Plagi za Volti 230 za AC, Amp 32
Tumia plagi ili kuendesha vifaa vya umeme vya Volti 230 za
AC, msururu mmoja, 50 Hz vinavyohitaji hadi wati 5,000 (kW
5.0) katika umeme wa Amp 21.7.
Vituo vya USB vya DC vya Volti 5
Umeme wa upeo unaopatikana kwenye vituo vya USB ni Amp
2.1 kwa Volti 5. Kituo cha USB kinakuwezesha kuchaji tena
vifaa vingi vinavyotumia nishati ya USB kwa kupitia kebo ya
kuchaji ya USB (haijajumuishwa).
ILANI Ili kupata matokeo bora zaidi unapochaji vifaa vya
Apple, tumia kituo cha USB cha chini.
ILANI Ya kuchaji ITE (Information Technology Equipment
[Kifaa cha Teknolojia ya Maelezo]) pekee.
Utumizi wa Nishati
Kifuatiliaji utumizi wa nishati kinaonyesha asilimia ya utumizi
jumla wa jenereta kwa kutumia LED (taa) 4.
TAA
RANGI
1
Kijani
2
Kijani
3
Manjano
4
Nyekundu inayokonyeza
4
Nyekundu imara
Uwekaji Upya Utumizi Kupita Kiasi
Ikiwa jenereta imetumika kupita kiasi, inakata nishati kwenye
vituo. Zima na uondoe vifaa vyote vinavyotumia umeme.
Bonyeza kitufe cha UWEKAJI UPYA UTUMIZI KUPITA KIASI
(OVERLOAD RESET), weka tena vifaa vinavyotumia umeme
moja baada ya kingine ili kuendelea kutumia kawaida.
KIFAA
0-≥25%
≥50%
≥75%
100%
Inatumia Kupita Kiasi
7

Quicklinks ausblenden:

Werbung

Inhaltsverzeichnis
loading

Inhaltsverzeichnis