Herunterladen Inhalt Inhalt Diese Seite drucken

Briggs & Stratton Q6500 Anleitung Seite 198

Inhaltsverzeichnis

Werbung

Verfügbare Sprachen
  • DE

Verfügbare Sprachen

  • DEUTSCH, seite 44
Hatua ya 2: Oili na Mafuta
Mapendekezo ya Oili Kielelezo 2
Tunapendekeza matumizi ya oili Zilizoidhinishwa na Hakikisho
la Briggs & Stratton ili kupata utendakazi bora. Oili nyingine za
usafishaji zinakubalika ikiwa zimebainishwa kwa huduma ya SF
au ya juu zaidi. Usitumie vitegemezi maalum.
Hali joto ya nje inaamua mnato sahihi wa oili kwa injini.
Tumia chati kuchagua mnato bora zaidi kwa hali joto ya nje
inayotarajiwa.
* Chini ya 4°C (40°F) matumizi ya SAE 30 yatasababisha
ugumu wa kuwasha.
** Zaidi ya 27°C (80°F) matumizi ya 10W30 huenda
yakasababisha matumizi zaidi ya oili. Kagua kiwango cha oili
mara nyingi zaidi.
Kukagua/Kuongeza Oili ya Injini Kielelezo 3 4 5
Kiwango cha oili kinafaa kukaguliwa kabla ya kila matumizi au
angalau kila baada ya saa 8 za uendeshaji. Dumisha kiwango
cha oili.
1. Hakikisha jenereta iko kwenye eneo tambarare.
2. Legeza skrubu tatu za kifuniko cha kando cha udumishaji
na uondoe kifuniko (3).
3. Safisha eneo linalozingira tundu la kujazia oili na uondoe
kifaa cha kupima kiwango cha oili.
4. Hakikisha oili imefikia alama inayoonyesha imejaa (full) (5,
A) (tundu la juu) kwenye kifaa cha kupima kiwango cha
oili.
5. Ikiwa inahitajika, ukitumia faneli, weka oili polepole ndani
ya tundu la kujazia (4) oili hadi ifikie alama inayoonyesha
imejaa (full) (5, A) (tundu la juu) kwenye kifaa cha kupima
kiwango cha oili.
ILANI Acha ili kuruhusu oili kutulia. Pangusa kifaa cha kupima
kiwango cha oili kila mara kiwango cha oili kinapokaguliwa.
USIJAZE kupita kiasi.
6. Funika na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili.
7. Funika kifuniko cha udumishaji na ukaze skrubu kwa
mikono.
ILANI Usijaribu kuwasha au kuanzisha injini kabla
haijafanyiwa huduma vizuri kwa kutumia oili inayopendekezwa.
Hii inaweza kusababisha injini kuharibika.
Ongeza Mafuta Kielelezo 6 7
Mafuta ni lazima yatimize mahitaji haya:
• Petroli safi, freshi, isiyo na risasi (unleaded) na iliyo na
angalau RON 91 (okteni 87/87 AKI).
• Petroli iliyo na hadi ethanoli 10% inakubalika.
ILANI Usichanganye oili kwenye petroli au kurekebisha
injini ili itumie mafuta mbadala. Usitumie petroli ambayo
haijaidhinishwa kama vile E15 na E85. Utumizi wa mafuta
ambayo hayajaidhinishwa kunaweza kusababisha uharibifu
kwenye jenereta na kubatilisha hakikisho.
Tazama Mwinuko wa Juu kwa mita 1,524 na zaidi.
ONYO! Mafuta na mivuke yake
yanaweza kuwaka moto na kulipuka
na kusababisha kuchomeka, moto au
mlipuko na kupelekea kifo au majeraha mabaya.
• Usiongeze mafuta wala kusongeza wakati inatumika.
• Zima injini na uwache injini ipoe kwa angalau dakika 2 kabla
ya kuondoa kifuniko cha mafuta.
• Jaza tangi la mafuta ukiwa nje ya nyumba. Usimwage mafuta
nje ya tangi.
6
• Weka mafuta mbali na cheche, moto ulio wazi, taa za gesi,
joto, na vyanzo vingine vya mwako.
• Kagua mifereji ya mafuta, tangi, kifuniko, na vijenzi mara kwa
mara kama kuna nyufa au uvujaji. Badilisha kama itahitajika.
• Usiwashe sigara wala usivute sigara.
• Usimwagilie jenereta maji ili kuzima moto.
• Tumia tu kizima moto kilichotengenezwa kuzima moto wa
mafuta na mifumo ya mifumo ya kiumeme kama vile kizima
moto cha poda. Fuata maagizo yaliyotolewa na mtengenezaji
wa kizima moto kabla ya matumizi.
• Jenereta hii haipaswi kutumiwa katika mazingira yanayoweza
kushika moto kwa urahisi.
1. Ondoa polepole kifuniko cha mafuta (6, A) ili kupunguza
shinikizo ndani ya tangi.
2. Polepole ongeza mafuta yasiyo na risasi (unleaded)
katika tangi la mafuta. Kuwa mwangalifu usijaze hadi juu
ya ukingo (7). Hii inawacha nafasi ya kutosha kwa ajili ya
upanuzi wa mafuta.
3. Rudisha kifuniko cha tangi la mafuta na uruhusu mafuta
yoyote yaliyomwagika kuyeyuka kabla ya kuwasha injini.
Mwinuko wa Juu
Katika mwinuko zaidi ya mita 1524, kiwango cha chini zaidi
cha RON 89 (okteni 85/85 AKI) cha mafuta kinakubalika. Ili
kudumisha uambatanaji na sera ya mafukizo, marekebisho ya
mwinuko wa juu yanahitajika. Uendeshaji bila marekebisho
haya unaweza kusababisha kupunguka kwa utendakazi,
matumizi ya mafuta kuongezeka, na mafukizo kuongezeka.
Mtembelee muuzaji wa Briggs & Stratton Aliyeidhibishwa ili
kupata maelezo kuhusu marekebisho ya mwinuko wa juu.
Uendeshaji injini katika mwinuko wa chini ya mita 762 na
marekebisho ya mwinuko wa juu hayapendekezwi.
Kusafirisha
Unaposafirisha mtambo ukitumia gari ama trela, weka swichi
ya injini hadi eneo linaloonyesha ZIMA (OFF) (0). Usiinamishe
injini au kifaa katika mkao unaosababisha mafuta kumwagika.
Kiashiria Oili Chache
Mfumo wa kiashiria oili chache umeundwa ili kuzuia
uharibifu wa injini unaosababishwa na oili isiyotosha ya injini.
Iwapo kiwango cha oili kimepungua hadi chini ya kiwango
kilichowekwa, taa nyekundu ya kiashiria oili chache itawaka na
swichi ya kiwango cha oili itazima injini. Iwapo injini itazima au
taa nyekundu ya kiashiria oili chache itawaka unapovuta mpini-
nywea, kagua kiwango cha oili ya injini.
Hatua ya 3: Kuanzisha Jenereta Kielelezo
ILANI Kila wakati ZIMA (0) swichi ya QPT unapoanzisha au
kuzima jenereta au unapotumia vituo vya USB vya DC.
Ondoa vyombo vyote vya umeme vilivyounganishwa na
jenereta. Tumia maagizo yafuatayo ya kuwasha:
1. Hakikisha kifaa kiko nje kwenye eneo tambarare.
ILANI Kukosa kutumia kifaa hiki kwenye eneo tambarare
kunaweza kusababisha kifaa kuzima.
2. Vuta nje kidhibiti cha choki (1, J) ili kufunga choki (
ILANI Kwa injini moto, hakikisha wenzo wa choki uko katika
eneo linaloonyesha ENDESHA (RUN) (
3. Zungusha swichi ya injini (1, K) hadi eneo linaloonyesha
WASHA (ON) (I).
4. Kamata mpini-nywea (1, G) na uvute polepole mpaka uhisi
ugumu kidogo. Kisha vuta kwa haraka ili kuwasha injini.
5. Fungua choki kwa utaratibu injini inaposhika joto kwa
kusukuma choki ndani.
).
BRIGGSandSTRATTON.COM
1
).

Quicklinks ausblenden:

Werbung

Inhaltsverzeichnis
loading

Inhaltsverzeichnis