Herunterladen Inhalt Inhalt Diese Seite drucken

Briggs & Stratton P4500 Handbuch Seite 246

Inhaltsverzeichnis

Werbung

Verfügbare Sprachen
  • DE

Verfügbare Sprachen

  • DEUTSCH, seite 54
Eneo la Kuendeshea ili Kupunguza Hatari ya Moto
ONYO! Joto/gesi za Eksozi zinaweza
kuwasha vitu, majengo au tangi la
mafuta lililoharibika zinazoweza kushika
moto, na kusababisha kifo au majeraha mabaya.
• Ni lazima jenereta ya kubebeka iwe angalau mita 1.5
mbali na jengo lolote, vitu vinavyoning'inia, miti, vichaka
au mimea yenye urefu wa zaidi ya sentimita 30.5.
• Usiweke jenereta ya kubebeka chini ya deki au aina
nyingine yoyote ya jengo ambalo litazuia hewa nyingi
kupita. Ving'ora vya moshi ni lazima viwekwe na
kudumishwa ndani ya nyumba kulingana na maagizo/
mapendekezo ya mtengenezaji.
• Ving'ora vya kaboni monoksidi haviwezi kugundua moshi.
• Usiweke jenereta ya kubebeka kwa njia nyingine
isipokuwa ambavyo imeonyeshwa.
Zaidi ya mita 1.5
Ekzosi
MUFFLER
Zaidi ya
mita 1.5
Hatua ya 2: Oili na Mafuta
Mapendekezo ya Oili Kielelezo
Tunapendekeza matumizi ya oili Zilizoidhinishwa na
Hakikisho la Briggs & Stratton ili kupata utendakazi
bora. Oili nyingine za usafishaji zinakubalika ikiwa
zimebainishwa kwa huduma ya SF au ya juu zaidi.
Usitumie vitegemezi maalum.
Hali joto ya nje inaamua mnato sahihi wa oili kwa injini.
Tumia chati kuchagua mnato bora zaidi kwa hali joto ya
nje inayotarajiwa.
* Chini ya 4°C (40°F) matumizi ya SAE 30 yatasababisha
ugumu wa kuwasha.
** Zaidi ya 27°C (80°F) matumizi ya 10W30 huenda
yakasababisha matumizi zaidi ya oili. Kagua kiwango cha oili
mara nyingi zaidi.
Kukagua/Kuongeza Oili ya Injini Kielelezo
Kiwango cha oili kinafaa kukaguliwa kabla ya kila
matumizi au angalau kila baada ya saa 8 za uendeshaji.
Dumisha kiwango cha oili.
1. Hakikisha jenereta iko kwenye eneo tambarare.
2. Zungusha kidude na ufunue kifuniko (5) kilicho juu
ya eneo la kujazia oili.
3. Safisha eneo linalozingira tundu la kujazia oili na
uondoe kifaa cha kupima kiwango cha oili.
4. Hakikisha oili imefikia alama inayoonyesha imejaa
(6, A) kwenye kifaa cha kupima kiwango cha oili.
5. Ikiwa inahitajika, ukitumia faneli, weka oili polepole
ndani ya tundu la kujazia oili (7) hadi ifikie alama
inayoonyesha imejaa (6, A) kwenye kifaa cha
kupima kiwango cha oili.
ILANI Acha ili kuruhusu oili kutulia. Pangusa kifaa
cha kupima kiwango cha oili kila mara kiwango cha oili
kinapokaguliwa. USIJAZE kupita kiasi.
6
Zaidi ya mita 6.1
4
5 6 7
6. Funika na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili.
7. Rejesha kifuniko kilicho juu ya eneo la kujazia oili.
ILANI Usijaribu kuwasha au kuanzisha injini
kabla haijafanyiwa huduma vizuri kwa kutumia oili
inayopendekezwa. Hii inaweza kusababisha injini
kuharibika.
Ongeza Mafuta Kielelezo
Mafuta ni lazima yatimize mahitaji haya:
• Petroli safi, freshi, isiyo na risasi (unleaded) na iliyo
na angalau RON 91 (okteni 87/87 AKI).
• Petroli iliyo na hadi ethanoli 10% inakubalika.
ILANI Usichanganye oili kwenye petroli au kurekebisha
injini ili itumie mafuta mbadala. Usitumie petroli ambayo
haijaidhinishwa kama vile E15 na E85. Utumizi wa
mafuta ambayo hayajaidhinishwa kunaweza kusababisha
uharibifu kwenye jenereta na kubatilisha hakikisho.
Tazama Mwinuko wa Juu kwa mita 1,524 na zaidi.
ONYO! Mafuta na mivuke yake
yanaweza kuwaka moto na
kulipuka na kusababisha
kuchomeka, moto au mlipuko na kupelekea kifo au
majeraha mabaya.
• Usiongeze mafuta wala kusongeza wakati inatumika.
• Zima injini na uwache injini ipoe kwa angalau dakika 2
kabla ya kuondoa kifuniko cha mafuta.
• Jaza tangi la mafuta ukiwa nje ya nyumba. Usimwage
mafuta nje ya tangi.
• Weka mafuta mbali na cheche, moto ulio wazi, taa za
gesi, joto, na vyanzo vingine vya mwako.
• Kagua mifereji ya mafuta, tangi, kifuniko, na vijenzi
mara kwa mara kama kuna nyufa au uvujaji. Badilisha
kama itahitajika.
• Usiwashe sigara wala usivute sigara.
• Usimwagilie jenereta maji ili kuzima moto.
• Tumia tu kizima moto kilichotengenezwa kuzima moto
wa mafuta na mifumo ya mifumo ya kiumeme kama
vile kizima moto cha poda. Fuata maagizo yaliyotolewa
na mtengenezaji wa kizima moto kabla ya matumizi.
• Jenereta hii haipaswi kutumiwa katika mazingira
yanayoweza kushika moto kwa urahisi.
1. Ondoa polepole kifuniko cha mafuta (1, J) ili
kupunguza shinikizo ndani ya tangi.
2. Polepole ongeza mafuta yasiyo na risasi (unleaded)
kufikia kiashiria cha kiwango cha mafuta (8, A)
katika tangi wa mafuta. Kuwa mwangalifu usijaze
hadi juu ya kiashiria. Hii inawacha nafasi ya kutosha
kwa ajili ya upanuzi wa mafuta.
3. Rudisha kifuniko cha tangi la mafuta na uruhusu
mafuta yoyote yaliyomwagika kuyeyuka kabla ya
kuwasha injini.
Mwinuko wa Juu
Katika mwinuko zaidi ya mita 1524, kiwango cha
chini zaidi cha RON 89 (okteni 85/85 AKI) cha mafuta
kinakubalika. Ili kudumisha uambatanaji na sera ya
mafukizo, marekebisho ya mwinuko wa juu yanahitajika.
Uendeshaji bila marekebisho haya unaweza kusababisha
kupunguka kwa utendakazi, matumizi ya mafuta
kuongezeka, na mafukizo kuongezeka.
Mtembelee muuzaji wa Briggs & Stratton Aliyeidhibishwa
ili kupata maelezo kuhusu marekebisho ya mwinuko wa
juu. Uendeshaji injini katika mwinuko wa chini ya mita 762
na marekebisho ya mwinuko wa juu hayapendekezwi.
1 8
BRIGGSandSTRATTON.COM

Quicklinks ausblenden:

Werbung

Inhaltsverzeichnis
loading

Diese Anleitung auch für:

030806-00

Inhaltsverzeichnis