Herunterladen Inhalt Inhalt Diese Seite drucken

Briggs & Stratton P2400 Bedienungsanleitung Seite 253

Inhaltsverzeichnis

Werbung

Verfügbare Sprachen
  • DE

Verfügbare Sprachen

  • DEUTSCH, seite 54
Briggs & Stratton inakubali, katika kipindi cha udhamini ulioelezwa hapa, itakarabati au badilisha, bila ya malipo, sehemu yoyote ilio na shida katika vifaa au
operesheni au zote. Bei ya kusafirisha bidhaa zilizotumwa ili zikarabatiwe au zibadilishwe kwa mujibu wa udhamini huu ni lazima mwenyewe agharamie. Udhamini
huu ni bora na unao uhusiano na vipindi vya muda na hali zilizotajwa hapa chini. Kwa huduma ya dhamana, tafuta Muuzaji wa Huduma Aliyeidhinishwa katika
ramani ya kielekeza wauzaji katika www.SimplicityMfg.com. Mnunuzi lazima awasiliane na Mwuzaji wa Huduma Aliyeidhinishwa, na kumpelekea mwuzaji huyo wa
Huduma Aliyeidhinishwa kwa ukaguzi na upimaji.
Hakuna udhamini ingine ya haraka. Udhamini ulioashiriwa, pamoja na zile za uuzaji na uzima fulani kwa lengo fulani, zina upungufu wa muda
uliosemwa hapo chini, au kwa kiasi kilichoruhusiwa na sheria. Hasara inayotokana na uharibifu wa kisadfa au unaosababishwa na sababu zinazojulikana
hazijajumuishwa kwenye kiwango cha kutojumuishwa ambacho kinaruhusiwa na sheria. Baadhi ya mataifa au nchi haziruhusu ufinyu wa kwa muda gani udhamini
uliorejelewa unadumu, na baadhi ya mataifa au nchi haziruhusu kutojumuishwa au upungufu wa hasara ya sadfa au inayotokana na hali fulani, ili upungufu
uliotajwa hapo juu na kutojumuishwa huenda kusitumike kwako. Udhamini huu unakupa haki mahsusi za kisheria na unaweza pia kuwa na haki nyingine ambazo
zinaweza kutofautiana kutoka katika taifa hadi taifa au nchi hadi nchi.**
▲ Betri (imewezeshwa) kwa matumizi ya nyumbani ya miezi mitatu wala sio ya kibiashara.
** Nchini Australia- Bidhaa zetu zinanunuliwa kwa udhamini ambao hauwezi kujumuishwa kulingana na Sheria ya Mtumizi ya Australia. Unastahili kusawazishiwa au
kurudishiwa hela zako kwa kushindikana kukubwa na kwa kufidhia kwa upungufu au hasara yoyote nyingine inayoweza kutabirika kwa njia ya kueleweka. Una haki
pia ya kutengenezewa au kubadilishiwa kama bidhaa haziko na ubora unaokubalika na uharibifu hauleti hasara kubwa. Kwa huduma ya udhamini, tafuta muuzaji
aliyethibitishwa na aliyekaribu na wewe katika ramani yetu kwa tovuti ya BRIGGSandSTRATTON.COM, au piga simu 1300 274 447, au kwa barua pepe au barua
kwa salesenquiries@briggsandstratton.com.au, Briggs & Stratton Australia Pty Ltd, 1 Moorebank Avenue, NSW, Australia, 2170.
Kipindi cha udhamini huanza tarehe ya ununuzi ya duka la kwanza au biashara la kwanza. "Matumizi ya kibinafsi" inamaanisha matumizi ya nyumbani na mnunuzi
wa rejareja. "Matumizi ya kibiashara" inamaanisha matumizi mengine yote, pamoja na matumizi ya kibiashara, ya kuzalisha mapato au kwa madhumunia ya
kukodisha. Pindi tu bidhaa imepitia matumizi ya biashara, itaweza kuchukuliwa kuwa bidhaa ya matumizi ya kibiashara kwa makusudio ya udhamini huu.
Hifadhi vyema ithibati yako ya risiti ya ununuzi. Ikiwa hutatoa ushahidi wa tarehe ya awali ya ununuzi katika wakati ambao huduma ya dhamana imetakiwa, tarehe
ya utengezaji wa bidhaa hio itatumika kuamua kipindi cha dhamana. Usajili wa bidhaa hauitajiki katika kupokea huduma ya udhamini kwenye bidhaa za
Briggs & Stratton.
Huduma ya udhamini inapatikana tu kupitia katika Wauzaji wa Huduma Walioidhinishwa kutoka Briggs & Stratton. Marekebisho nyingi ya udhamini yanafanwya
mara kwa mara, lakini wakati mwingine maombi ya huduma ya udhamini yanaweza kuwa sio sahihi. Dhamana hii inajumuisha tu dosari katika nyenzo au ustadi.
Haijumuishi hasara au uharibifu unaosababishwa na matumizi yasiyofaa au matumizi mabaya, ukarabati usiofaa au utengenezaji, kuchujuka kwa kawaida au
mafuta mabaya au ambayo hayajaidhinishwa.
Matumizi Mabaya na Dhuluma - Matumizi sahihi ya bidhaa hii yameelezwa katika Mwongozo wa fundi. Kwa kutumia bidhaa hii kwa njia ambayo haijafafanuliwa
katika Kabrasha la Mtumiaji au kwa kutumia bidhaa hii baada ya kuharibika hakutajumuishwa katika udhamini huu. Kujumuishwa kwa udhamini huu hakutaweza
kutolewa pia kama nambari ya usajili kwenye bidhaa hii imeondolewa au bidhaa hii ina kasoro au imebadilishwa kwa njia yoyote, au kama bidhaa hii inayo ithibati
ya matumizi mabaya kama vile uharibifu mbaya au uharibifu unaotokana na kuchunjika kwa maji/kemikali.
Ukarabati au Urekebishaji Mbaya - Bidhaa hii lazima ikarabatiwe kwa mujibu wa taratibu na ratiba zinazotolewa katika mwongozo wa fundi, na kuhudumiwa au
kurekebishwa kwa kutumia sehemu halisi za Briggs & Stratton. Uharibifu unaosababishwa na ukosefu wa ukarabati au matumizi ya vipuri viso-asilia haujajumuishwa
katika udhamini huu.
Uchakavu wa Kawaida - Kama mitambo nyingi, bidhaa yako itakuwa na uchakavu hata kama inakarabatiwa kwa sahihi. Udhamini huu haujumuishi ukarabati
wakati ambapo matumizi ya kawaida yamesababisha kuchujuka kwa sehemu ya mtambo huu au mtambo wowote. Ukarabati na vitu vinavyochujuka kama vile
vichungio, mishipi, mundu(blades) za kukatia, na padi za breki (isipokuwa padi za breki za injini) vyote havijajumuishwa kwenye udhamini kutokana na kipengele
cha kuchujuka pekee, isipokuwa endapo sababu itakuwa kasoro kwenye nyenzo au utengenezwaji wake.
Mafuta Yaliyooza au Hayadhibitishwa - Ili bidhaa hii ifanye kazi ipasavyo, inahitaji mafuta safi inayoendanisha na vigezo vilivoelezwa katika Mwongozo wa Fundi.
Uharibifu wa injini au mtambo uliosababishwa na mafuta mabaya au matumizi ya mafuta hayajaidhinishwa (kama vile E15 au E85 ethanol blends) hayajajumuishwa
kwenye udhamini huu.
Zilizotengwa - Udhamini huu hauzingatii uharibifu kutokana na ajali, unyanyasaji, marekebisho, mabadiliko, huduma mbaya, kugandisha au kuzorota kutokana
na kemikali. Viambatisho au nyongeza ambavyo havikuunganishwa asilia kwenye bidhaa hii vyote havijajumuishwa pia. Hakuna udhamini kwa vifaa vinavyotumika
kwa nguvu ya msingi badala ya nguvu ya kutumika au juu ya vifaa vya kutumika kuokoa maisha. Udhamini huu hauzingatii injini au vifaa vilivyotumika, badilishwa
muundo, mitumba, au za kujaribia. Udhamini huu haujumuishi pia kushindikana kunakotokana na vitendo vya Mungu na nguvu nyingine ya matukio yaliyo zaidi ya
udhibiti wa mtengenezaji.
SERA YA UDHAMINI WA BIDHAA ZA BRIGGS & STRATTON
Udhamini Pungufu
KIPINDI CHA DHAMANA
Matumizi ya Kibinafsi
Miezi 36 ▲
KUHUSU DHAMANA YAKO
Matumizi ya Kibiashara
Miezi 12
80088366SW (Rev. A)
13

Quicklinks ausblenden:

Werbung

Inhaltsverzeichnis
loading

Inhaltsverzeichnis