Herunterladen Inhalt Inhalt Diese Seite drucken

Briggs & Stratton P2400 Bedienungsanleitung Seite 250

Inhaltsverzeichnis

Werbung

Verfügbare Sprachen
  • DE

Verfügbare Sprachen

  • DEUTSCH, seite 54
Uhifadhi
Ikiwa unahifadhi kifaa hiki kwa zaidi ya siku 30, tumia
miongozo ifuatayo ili kukiandaa kwa uhifadhi.
Maagizo ya Uhifadhi wa Muda Mrefu Kielelezo
1. Safisha jenereta kama ilivyoainishwa kwa Kusafisha.
2. Badilisha oili ya injini wakati injini ingali na
joto, mwaga mafuta utoka kwenye kifuniko cha
kasha la shafti kombo. Jaza ukitumia ya ubora
unaopendekezwa. Tazama Kubadilisha Oili ya Injini.
3. Tibu au umwage mafuta kutoka kwenye
jenereta kwa sababu mafuta yanaweza kuganda
yanapohifadhwa kwa zaidi ya siku 30.
Mafuta yaliyoharibika yanaweza kusababisha mabaki ya
asidi na gundi kutengenezeka kwenye mfumo wa mafuta
au kwenye sehemu muhimu za kabureta. Ili kuweza
mafuta yakiwa safi, tumia kisawazishaji mafuta.
Hakuna haja ya kumwaga petroli kutoka kwenye injini
ikiwa kiimarishaji mafuta kimeongezwa kulingana
na maagizo. Washa injini kwa dakika 2 kuzungusha
kisawashaji katika mfumo wote wa mafuta kabla ya
kukiweka.
Ikiwa petroli ndani ya injini haijatibiwa kwa kiimarishaji
mafuta, ni lazima imwagwe kwenye kontena
iliyoidhinishwa. Kisha uendeshe injini hadi isimame
kutokana na ukosefu wa mafuta. Matumizi ya kiimarishaji
mafuta kwenye kontena ya uhifadhi yanapendekezwa ili
kudumisha usafi.
ONYO! Mafuta na mivuke yake yanaweza
kuwaka moto na kulipuka na kusababisha
kuchomeka, moto au mlipuko na kupelekea kifo
au majeraha mabaya.
• Unapohifadhi mafuta au kifaa chenye mafuta kwenye
tangi, hifadhi mbali na tanuu, stovu, hita za kuchemshia
maji, vifaa vya kukausha nguo au vitu vingine ambavyo
vina taa za moto au vyanzo vya mwako kwa sababu
vinaweza kuwasha moto kwenye mivuke ya mafuta.
• Unapomwaga mafuta, zima injini na uwache injini
ipoe kwa angalau dakika 2 kabla ya kuondoa kifuniko
cha mafuta. Legeza kifuniko hicho polepole ili kutoa
shinikizo kwenye tangi. Mwanga mafuta ukiwa nje ya
nyumba. Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi,
taa za gesi, joto, na vyanzo vingine vya mwako.
• Kagua mifereji ya mafuta, tangi, kifuniko, na vijenzi
mara kwa mara kama kuna nyufa au uvujaji. Badilisha
kama itahitajika.
4. Zungusha kidude cha kugurumisha (K) hadi eneo
linaloonyesha zima (0)
5. Hifadhi jenereta katika mahali safi na pakavu na
uifunike ukitumia kinga mwafaka ambayo haitasitiri
unyevunyevu.
ONYO! Vifuniko vya uhifadhi vinaweza
kusababisha moto na hatimaye kifo au
majeraha mabaya.
• Usiweke kifuniko cha uhifadhi juu ya jenereta ambayo
ni moto au inayoguruma. Subiri vifaa vipoe kwa muda
tosha kabla ya kuweka kifuniko juu yake.
10
1
BRIGGSandSTRATTON.COM

Quicklinks ausblenden:

Werbung

Inhaltsverzeichnis
loading

Inhaltsverzeichnis